HabariSiasa

Bilioni 1.6 zatolewa kufadhili wanafunzi Zannzibar

Mkurugenzi wa City college of Health Ilala Campus/ KILIMANJARO INSTITUTE of Health Shabani Mwanga ametoa ufadhili wa zaidi ya bilioni 1.6 kwa wanafunzi wa Zanzibar, makubaliano hayo yamefanyika kati ya wizara ya Elimu na mafunzo ya amali ZANZIBAR tarehe 05.06.2023.

Makubaliano hayo yamesainiwa na katibu mkuu wizara ya elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Khamis Abdullah na Mkurugenzi wa city college of Health/KILIMANJARO INSTITUTE of Health ndugu Shabani Mwanga katika ukumbi wa Wizara hiyo Mazizini Zanzibar.
“Lengo kubwa ni kuhakikisha tunatoa ufadhili wenye tija kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar ili kuendena na kasi ya Uchumi wa buluu ambapo zaidi ya Bilioni 1.6 zitatumika kuwafadhili wanafunzi Hao ambao ni 230″Shabani Mwanga.

Pamoja na hayo Shabani mwanga alisema wamehamasika kutoa ufadhili huo kutoka na mashirikiano makubwa yaliyopo kati ya vyuo vya city college/KILIMANJARO INSTITUTE OF HEALTH na viongozi wa Wizara mbalimbali za Zanzibar hususani Wizara ya Elimu wakiwemo mazwaziri na makatibu wakuu wa wizara hizo.

Naye katibu mkuu wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Khamis Abdullah kwa niaba ya serikali ya mapinduzi Zanzibar alishukuru ufadhili huo mkubwa kwa wanafunzi wa Zanzibar na kuwataka wanafunzi na wazazi wajitahidi kuomba nafasi hizo kupitia Wizara ya elimu na mafunzo ya Amali mapema iwezekanavyo.
“Kwetu sisi kama Wizara kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mkurugenzi wa city college of Health/KILIMANJARO INSTITUTE of Health ndugu Shabani Mwanga kwa kuona umuhimu wa kutoa ufadhili huu kwa wanafunzi wa Zanzibar kwani idadi ya wanafunzi 230 ni kubwa sana na italeta faraja kwa wazazi na wanafunzi.
Katibu mkuu alitoa ahadi ya kushirikiana na vyuo vya City college/KILIMANJAROINSTITUTEOFHEALTH kuwapatia wanafunzi maeneo ya kufanya mafunzo kwa vitendo pale inapohitajika bila kizuizi chochote”Khamis Abdulla.

Baada ya hafla hiyo kufanyika Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Lela Mohamed Mussa alipata fursa ya kuzungumza na uongozi wa city college of Health Ilala Campus na kuwapongeza kwa ufadhili huo mkubwa wa wanafunzi 230.
Lela aliahidi ushirikiano wa hali ya juu kati ya wizara yake na chuo na kuwataka waendelee Kuja Zanzibar kwani bado uwekezaji unahitajika hususani sekta ya elimu na Afya.

City college of Health/KILIMANJARO INSTITUTE of Health wamekuwa watu wa karibu sana katika maendeleo ya Zanzibar hususani sekta ya elimu,afya na michezo kitendo kinachochochea maendeleo ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents