Burudani

Billnass alipanga kumshirikisha Maua Sama kwenye Mazoea, aeleza jinsi Mwana FA alivyoingia

Maua Sama ndiye alikuwa amepangwa kushirikishwa kwenye wimbo Mazoea, kwa mujibu wa Billnass.

Akizungumza kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz, Bill alisema wimbo huo aliurekodi mwaka 2014 ambapo aliingiza verse mbili na chorus yake lakini akahitaji pia sauti za Maua Sama.

“Maua ni mshkaji wangu lakini ikija kwenye biashara mimi siletagi tena ushkaji, lazima nifuate management yake na nini. Kwahiyo nikamfuata Mwana FA nikamuambia nina demo ya wimbo wangu nataka uisikilize, sababu mara nyingi pia nyimbo zangu zote Mwana FA huwa nampa anasikiliza sababu naliamini pia sikio lake,” alisema Bill.

“Nilipompa Mwana FA akasema ‘Maua utampata lakini unaweza kuniachia CD ya huu wimbo ?’ Nikamwachia CD, long time. Wakati anaendelea kusikiliza akapata naona idea, akafanya, yeye sema alifanya mwaka jana. Nilikuwa surprised kwa jinsi ilivyofanyika na mtu kama FA kuweza kufanya verse kwa mapenzi bila mimi kumuomba labda, au mimi kumsumbua alijitolea, hapo tu mimi nikaaminia huu wimbo ni mzuri, unaweza kufanya kitu, na nilivyosikia ile verse ya Mwana FA ikabilisha wimbo.”

Mazoea ni miongoni mwa nyimbo zinazoendelea kufanya vizuri nchini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents