Bongo5 ExclusivesBurudaniHabariLifestyle

Billnass na Nandy wabarikiwa kupata mtoto wa kike

Kupitia ukurasa wa Instagram wa @billnass ambaye ndio baba wa mtoto ameandika kuwa:

“Ahsante Mungu Kwa zawadi na Baraka…kila iitwapo leo!! Kwangu Mimi 2022 ni Mwaka wa kipekee sana…nina kila sababu ya kushukuru na Kutoa Sadaka…Mungu Wetu ni Mwema Sana 🙏🏿🙏🏿🙏🏿 !! Pili Kipekee Niseme Ahsante Mke wangu Kipenzi @officialnandy Kwa Kuniletea Mrembo na Rafiki, Haikuwa Kazi Rahisi umenionesha wewe ni Shujaa kiasi gani kwanzia Mtoto akiwa tumboni mpaka Muda unajifungua umepigana sana… nimejionea namna gani mtu anaweza ku risk kupoteza uhai wake wakati wa kujifungua…Hii imefanya nizidi kukupenda, Kukuheshimu na kukupa Nafasi ya Pekee katika Maisha Yangu….Hayo Yote Hayatoshi Lakini Kila Siku Nakuombea Kwa Mungu akulinde Mke Wangu na Nitakupa Furaha Na Kufanya Maisha Yako Yawe ya Amani kwani Unastahili Mengi Mazuri sina zawadi kubwa itakayoweza lingana na Upendo wangu kwako zaidi ya kuzidisha upendo kila iitwapo leo ❤️❤️❤️ Nikuhakikishe uko Mikono Salama 🙏🏿🙏🏿🙏🏿 !!! Tatu kwa Mwanangu kipenzi Najuwa ipo siku utakuja kuisoma Hii…Niseme tu Nakupenda Sana sana na Umekuja na Baraka Nyingi ambazo siwezi hata kuzielezea…Mwenyezi Mungu akutunze kwa Mapenzi yake na Ukawe mtu mwema katika ulimwengu wa kawaida na wa kiroho… Na Pia nikupongeze umekuwa Balozi wa @assemble_insurance “

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents