Michezo
Bocco mchezaji mpya wa JKT Tanzania
Ni muda wa wapinzani kukaa roho juu ndivyo unavyoweza kusema baada ya klabu ya JKT Tanzania kumtambulisha John Rafael Bocco kutokea Simba SC.
Bocco ambaye ni mmoja wa wachezaji wenye rekodi za kutisha Ligi Kuu Bara aliachana na Simba mwisho mwa msimu uliopita ambapo alipewa of aya kufundisha timu za Vijana chini ya miaka 17.
Kwa utambulisho huo inamaanisha kuwa Bocco ataendelea kusakata kandanda msimu ujao 2024/2025 akiwa na JKT Tanzania.