Michezo

Bondia Ibrahimu Classic alamba dili nono, afunguka uhalisia wa maisha yake, pambano jipya sio siri tena

IBRAHIMU CLASS ATANGAZA PAMBANO LAKE KIMATAIFA NA KULAMBA UBALOZI LEO HII

 

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania na namba moja kwa sasa Afrika mashariki huku akishika nafasi ya pili Afrika nzima na nafasi ya 30 Duniani kwa uzito wa chini ya kilogram 60 @ibrahimuclass siku ya Leo amelamba ubalozi mwingine na kampuni ya @viwanja_nafuu PERFECT PROPERTY COMPANY LTD, @ibrahimuclass akiwa kama kioo cha jamii.


Mkurugenzi wa kampuni hiyo amefunguka juu ya sababu kubwa ya kumuona Ibrahim Class kama mtu pekee anayewafaa kama Balozi wao, ikumbukwe kampuni ya Perfect Property inajihusisha haswa na vitu (Mali) zisizohamishika mfano Ujenzi wa nyumba, ununuzi wa viwanja, mashamba utengenezaji wa hati miliki kwa urahisi, Ibrahim Class akiwa kama moja ya wateja wao wakaona ni vyema kumpa ubalozi Leo hii.

Pia Bondia @ibrahimuclass ametangaza rasmi kwamba hivi karibuni atakuwa na pambano la kimataifa kwahiyo mashabiki zake wakae kwa kujiandaa juu ya hilo, na pia kuahidi kutowaangusha mashabiki wake.

Kuangalia video kamili tembelea ukurasa wetu wa YouTube Bongo5.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents