BurudaniHabari

Bongo Fleva kutokuza wasanii wapya, Tatizo wasanii au mashabiki kuchagua wasanii??

Kupitia kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia tasnia ya muziki wa Bongo Fleva namna inavyokuza na kuzalisha wasanii wapya kila mwaka kama tasnia za muziki kwenye mataifa mengine zilivyo.

Annasema ni kweli Tanzania tuna bahati karibia kila mwaka wasanii wanazalishwa wapya na wanafanya vizuri ila tatizo linakuja hawakui.

Wengi wao wakitoa ngoma moja kuja kurudi tena imekuwa shida sana na hili tumeliona kwa wasannii wengi sana mfani, Lody Music, Bruce Afrika, Dayoo, Kontawa na hata Mavokali ambao walitoa nyimbo zimefannya vizuri sana.

Asilimia kubwa walitoa nyimbo zimefanya vizuri kweli lakini baadhi ndio unnawaona kwenye tasnia wakiendelea kufanya vizuri lakini baadhi yao huwasikii kabisa kama ilivyokuwa mwanzo.

Mbali na hilo wasanii baadhi kama Marioo, Jay Melody, Mbosso, Tommy Flavour, Ibraah na wengine huoni wakikua na kufanya harakati za kuufanya muziki uende mbali.

Wengi wao wanaonekana kuridhika na wakitoa nyimbo zikifanya vizuri na ku-trennd basi hakun a hatua zinngine wanazofanya kukuza muziki wao.

Wasanii wakubwa Tanzania wamebaki wale wale kwa zaidi ya miaka 15, hilo ni tatizo kwenye tasnia, huoni wasanii wapya watakaoleta changamoto kwa wasanii wakubwa.

Unahisi kuna tatizo sehemu gani katika kukuza wasanii wapya na kuwafanya kuja kuleta changamoto kwa wasanii wakubwa waliopo??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents