Makala

#Bongo5hamasa: Bila kujitoa bila maumivumi huwezi kuwa chochote

Kwenye maisha hakuna udungu wala urafiki bila kazi kwa maisha ya sasa, ukiwa, watu wengi sana wamepambana kwenye maisha na kufanikiwa ingawa, kwa leo tunamtolea mfano staa wa Bongo Fleva ambaye amekuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii na vijana wengi kutoakana na aina ya maisha aliyopita na aina ya maisha anayoishi kwa sasa.

Diamond platinum anasema “Yaani nahangaika usiku kucha naambulia patupu nilikuwa naumia. Moyoni najipa moyo kesho nitakuwa maarufu mwisho wa siku nafulia”

Binadamu ni wimbo ambao anazungumzia “hustle” kabla hajawa habari mjini hapa. Mahangaiko aliyopitia muhimu hakukatatamaa miaka kumi nyuma siyo sawa na leo. Usikate tamaa pia hangaika jipe moyo. Kesho ipo.

Kesho yakupendeza ipo kwa wale tu wanaotoa machozi jasho na damu.
Yaani hivi bila Maumivu bila kujitoa huwezi kuwa chochote huwezi fika popote.

Tuendelee kuhangaika tena mpaka ndoto zetu ziwe kweli tusikate tamaa na kuziachilia hakuna mwingine anayejali.

Inauma sana kuhangaika na kuambulia patupu lakini inauma zaidi kukata tamaa kisha miaka 2 au 5 unajikuta palepale ulipo kuwa leo. Tupambane kama leo tunapiga vizinga kesho itukute tunavyetu.

Imeandaliwa na @tujuavyo and @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button