Makala

#Bongo5Hamasa: Hakuna atakayekuletea unachokitaka, amka upambane

Sitasahau!,kauli hii aliyonukuliwa gwiji wa reggae Tanzania marehemu Justin Kalikawe kwenye jarida la maisha
jinsi tuyajuavyo inasema.

“HAKUNA, atakaye kuja kukufanyia kile utakacho ukifanye. HAKUNA , atakaye kuja kukuletea kile utakacho ukipate. Itabidi ufanye mwenyewe”

Unaposikia kauli hii, inakuelekeza UNAWAJIBIKA na maisha yako. Hakuna mwingine ila wewe mwenyewe anayeweza kufanya kile utakacho kifanyike, hata sasa bado hakijafanyika kwa sababu bado hujafanya. Hakuna atakaye kuletea kile utakacho ukipate.

Okk sawa watu wana weza kukupa vitu , hawawezi kukupa vitu unavyohitaji ,bora kutafuta unachotaka kuliko kupewa usichohitaji.

Kumbuka marazote kuwa ni wewe unaye wajibika hautakuwa na muda wakulaumu wengine kwa shida zako, hautakuwa na nguvu za kutengeneza visingizio kuwa unaonewa au upo hivyo sababu hukusaidiwa.

Tunapata kielelezo kingine toka kwa Albert Ellis aliyesema “wakati mzuri wa maisha yako ni pale unapotambua kuwa matatizo yako ni yako na wala si ya mama yako au raisi wako”
Katika hali yo yote ile inatupasa kuwajibika na maisha na hatma zetu.

Anza kuwajibika na maisha yako
#Bongo5hamasa
Imeandaliwa na @tujuavyo 

Related Articles

Back to top button