Makala

#Bongo5Hamasa: Kama kuna jambo unalifanya huoni changamoto jua unakosea

Kwa miaka 6 Siddhartha Gautama alitafuta jibu la kitendawili cha maisha alipata mafunuo na kuwa “Buddha” ikimaanisha “aliyefunuliwa” au “mbarikiwa” alifunuliwa kuwa “maisha ya binadamu ndio maisha ya mateso au changamoto au huzuni yaani dukkha .

Kwenye maisha tunachangamoto nyingi mno kiasi cha kukosa hamu kuendelea . Vipindi vya changamoto huwa vifupi lakini ni vigumu mno kufaulu.

Huwezi kosa changamoto kabisa kabisa,hata kukosa changamoto ni changamoto pia. Kuoa ni changamoto,kuacha ni changamoto usipooa changamoto.

Kuanza biashara changamoto,kufunga changamoto,kukaa tu changamoto.kuzaa changamoto kukosa uzao changamoto pia.

Ikiwa huna changamoto,jiulize mana hata kufa changamoto ,maisha baada ya kifo nayo changamoto. kuishi kwenye ulimwengu huu wenye dhiki ni changamoto.

Turudi kwenye kauli ya Ruge aliyowahi kusema
” KAMA KUNA JAMBO UNAFANYA HALINA CHANGAMOTO ZOZOTE JUA KUNA MAHALI UNAKOSEA”

Ndio nakubaliana naye unaweza kusema,sio lazima niwe na changamoto. Kumbuka maana nyingine ya changamoto ni hamu ya kufanya kitu tunasema hamasa kama unafanya jambo ambalo huna hamasa ya kufanya ni changamoto kama hujui.

#Bongo5hasama imeandaliwa na @tujuavyo na @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button