Makala

#Bongo5hamasa: Usichague kazi ya kufanya, njaa yako hakuna anayeijali

Siri ya kuyatokea maisha ukiwa huna kitu. Usichague cha kufanya wakati ndani huna chochote huna akiba huna jambo . Yaani huna hakika kama utakula ama la !! Lakini unajifungia ndani. Unachagua kazi.

Toka nje kama ni mitaro chimba kama ni saidia fundi komaa . Fanya unachoweza kukufanya uishi wakati unasubiri au unatafuta kazi unayostahili

Hata Cristiano Ronaldo alianzia chini kabisa kuna wakati alikuwa akifagia car parking ili aweze kumudu maisha. Pamoja na kuwa na ndoto kubwa ya kuwa mchezaji soka mkubwa na tajiri .

Hakuionea aibu njaa yake, hakuchagua kazi . Na sasa ndoto zake zimetimia.

Kama unaanzia from the scratch huna urithi huna bega la kuegemea. jipe moyo usichague kazi . Pambana mwisho utatoka.

Changamoto ni nyingi hasa Kama huna wa kukushika mkono kwa ujasiri weka mikono mfukoni chapa rapa🤣🤣.

Imeandaliwa na @tujuavyo & @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button