Makala

#Bongo5Nukuu: Yale usiyopenda kutendewa na wenzako nawe usiwatendee

Nukuu ya leo toka kwa Confucius,mwanafalsafa wa uchina. Confucius alitoka katika familia masikini,alilazimika kujitegemea yeye mwenyewa tokea utotoni.

Baba yake mzazi alifariki alipokuwa na umri wa miaka mitatu.Ugumu wa maisha na umasikini wa wakati ule ulimsaidia kuyafahamu vizuri maisha ya watu wa kawaida.

Jitihada na bidii yake ilikuwa kuwafanya wanadamu wawe watu bora katika maisha ya sasa .Confucius alisifiwa na kuheshimiwa na watu karibu sawa na mungu.

Mahekalu mengi yamejengwa kwa heshima yake katika kila jimbo China,pia walianzisha vyuo ambamo mambo muhimu ya confucius yalifundishwa. Msingi wa mafundisho yake umewekwa katika maneno haya

“Hayo usiyoyapenda kutendewa na wenzako,na wewe usiwatendee”

Kinafanana sana na alichokisema Yesu mahubiri ya mlimani

Mathayo 7
12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.

#Bongo5falsafa imeandaliwa na @tujuavyo and @el_mando_tz

Related Articles

Back to top button