HabariSiasa

Boris Johnson na Kagame wakutana kujadili uhamiaji wa wakimbizi

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amefanya mazungumzo na Rais wa Rwanda Paul Kagame Alhamisi kuhusu makubaliano yao ya uhamiaji ambao umezua mivutano mikali.

Nchi zote mbili zimetetea mpango huo, ambao unataka Uingereza kuhamisha wakimbizi walioko nchini kwake kwenda Rwanda.

Viongozi hao wawili wamepongeza ushirikiano wao wa uhamiaji na maendeleo ya kiuchumi ambayo yanakabiliana na usafirishaji hatari wa binadamu na kutoa fursa kujenga maisha mapya katika nchi salama, ofisi ya Johnson imesema hayo.

Mkutano wao pembeni ya mkutano wa Jumuiya ya Madola unafuatiwa na mazungumzo mjini Kigali Jumatano baina ya Kagame na Mwanamfalme wa Uingereza Charles ambaye aliripotiwa akisema kuwa mpango huo unasikitisha.

Makundi ya kutetea haki za binadamu, viongozi wa kanisa na Umoja wa Mataifa pia wamepinga mpango huo ambao ulitishia kugubika mkutano wa viongozi wa serikali wa Jumuiya ya Madola.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents