Bosi GSM aanika nguzo tatu Yanga kuwa Kimataifa

Katika kuhakikisha wanaifanikisha Young Africa Sports Club kuwa kwenye levo kubwa za Kimataifa, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Eng. Hersi Said amezitaja nguzo tatu za mafanikio katika klabu ya mpira wa miguu na kuahidi kuyajenga maeneo hayo kwa umakini, uweledi, uzalendo na mapenzi mema.

Eng. Hersi Said amesema katika kuhakikisha wanafikia malengo yao, basi watalazimika kujenga maeneo hayo matatu. ”Three PILLARS of a successful football CLUB are; 1. PROPER MANAGEMENT 2. GREAT TECHNICAL DEPARTMENT 3. TOP CLASS PLAYERS.’‘ ameandika Eng. Hersi Said

Mabosi hao wa Yanga kupitia GSM, ameongeza ”Katika kufikia malengo yetu, tunalazimika kujenga maeneo haya matatu kwa UMAKINI, UWELEDI, UZALENDO na MAPENZI MEMA kwa klabu yetu. AIDHA, ujenzi huu utafanyika katika muda mfupi tulionao bila kusita wala kutetereka. HESABU SIKU KUANZIA SASA KATIKA SAFARI HII itakayo wavutia sasa na hata vizazi vyetu hapo kesho.”

Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya raundi 37, ikiwa na pointi sawa na Azam huku wakitofautiana magoli ya kufunga na kufungwa.

Related Articles

Back to top button