Boss apigwa faini kisa kukataza likizo ya hedhi kwa wanawake

Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa shirika la ndege ambaye alikataa kuwaruhusu wafanyikazi wa kike kuchukua likizo ya hedhi iliyolindwa na sheria ya ajira ametozwa faini ya karibu $ 1,800 (Pauni 1,300) na mahakama moja huko Korea Kusini.

Kim Soo-cheon, mkuu wa zamani wa Shirika la ndege la Asiana, alikataa maombi 138 kutoka kwa wahudumu 15 wa ndege mnamo 2014 na 2015.

Bw Kim alidai wafanyakazi hawakutoa uthibitisho wa hedhi.

Tangu 1953, wanawake nchini Korea Kusini wameruhusiwa kuchukua likizo ya siku moja kwa mwezi ikiwa wana vipindi vya hedhi vyenye uchungu.

Likizo ya hedhi ni nini?

• Inaruhusu wanawake kuchukua siku moja au mbili za kupumzika kwa mwezi, wakati mwingine bila kulipwa, wanapokuwa katika kipindi chao

• Ipo katika nchi kadhaa, pamoja na Japan, Indonesia na Taiwan

• Hatahivyo, ni wanawake wachache ndio wanaoitumia

• wanaunga mkono likizo hiyo wanasema likizo ya hedhi ni muhimu kwa wanawake kama likizo ya uzazi, na kwa utambuzi wa mchakato wa kimsingi wa kibaolojia.

• Lakini wakosoaji wanasema inaimarisha maoni potofu ya wafanyakazi wa kike na inaweza hata kuwavunja moyo waajiri kukwepa kuajiri wanawake

Mahakama ya mwanzo ilimpata kwanza na hatia Bw Kim mnamo 2017. Alisema kuwa kulikuwa na “Visa vingi vya kutiliwa shaka” wakati wafanyikazi walipoomba likizo karibu na siku za likizo au siku za mapumziko, shirika la habari la Korea Kusini Yonhap linaripoti.

Hatahivyo, mahakama ilisema kuwa kuwataka wafanyakazi wathibitishe kuwa wako kwenye hedhi “kulikiuka faragha na haki zao za kibinadamu”.

Uamuzi huo uliungwa mkono na Mahakama ya juu.

Haki ya likizo ya hedhi nchini Japan imekuwepo kwa zaidi ya miaka 70, na nchi hiyo si peke yake katika Asia kwa kuwa na sera kama hiyo. Korea Kusini ilipitisha likizo hiyo mnamo 1953. Na nchini China na India, majimbo na kampuni zinazidi kupitisha sera za likizo ya hedhi na haki mbali mbali.

Hali katika upande wa pili wa ulimwengu, hata hivyo, inaonekana tofauti sana. Sera ya likizo ya hedhi haipo huko Marekani , Uingereza na Ulaya.

Na hata katika nchi ambazo zina likizo hiyo , wanawake wamegawanyika ikiwa ni hatua ya kurudi au ishara ya maendeleo linapokuja suala la haki za wanawake. Wengine wanasema kuwa ni muhimu kwa wanawake wanaofanya kazi kama likizo ya uzazi, wakati wengine wanasema kwamba inatoa taswira kwamba wanawake hawana uwezo kuliko wanaume na inaweza kusababisha ubaguzi zaidi.

Japan ilianzisha sera yake ya likizo hiyo katika kipindi cha 1947 ili kushughulikia masuala ya haki za wafanyakazi.

Kwa takribani muongo mmoja, wafanyakazi wa kiwanda wa kike walikuwa wamepewa likizo ya muda ili kuwapa ahueni kutokana na kazi ngumu na hali mbaya ya usafi, wakati wanapambana na maumivu ya hedhi.

Baada ya kushindwa kwa Japan katika Vita vya pili vya dunia nchi hiyo iliweka likizo ya hedhi katika sheria mpya za wafanyakazi kama haki kwa wafanyakazi wote wa kike ambao vipindi vyao ni “vigumu sana.”

Related Articles

Back to top button