Fahamu

Boti mpya ya Jeff Bezos haijawahi kutokea, ni ya kifahari zaidi (+ Video)

Habari kwamba Jeff Bezos amenunua boti walioiita “superyacht” . Wataalam wanasema biashara ya boti hizi imekuwa ikiongezeka kwa miaka, hata wakati wa kushuka kwa uchumi wa ulimwengu unaosababishwa na janga virusi vya corona.

Jeff Bezos, mwanzilishi wa Amazon , na mtu tajiri zaidi duniani, ameshuhudia utajiri wake ukichuoa mara mbili zaidi tangu mwaka 2017, mfuko wake ulituna zaidi mwaka jana kutokana na watu wengi zaidi kugeukia kwenye utaratibu wa manunuzi kupitia mtandao.

Si Bezos pekee. Matajiri wakubwa duniani wameshuhudia utajiri wao ukipanda miaka ya hivi karibuni.

Na kupitia hayo yote, soko la meli limeendelea kukua, wataalamu wanasema wakieleza linakua kubwa kadiri zinapopata umaarufu. Kulingana na wataalam na madalali, mwaka 2020 walishuhudia boti zaidi zikiuzwa kuliko hapo awali, na 2021 iliweka tena kuvunja rekodi za mauzo.

Tunachokifahamu kuhusu boti ya Bezos

Chombo hicho cha futi 416 (mita 127) kinatengenezwa Uholanzi na kampuni ya Oceanco, kwa mujibu wa wasifu mpya wa Bezos uliochapishwa na Bloomberg News.

Inakadiriwa kugharimu karibu dola za Kimarekani milioni 500, pesa ndogo sana mtu kama yeye tajiri zaidi duniani, ambaye utajiri wake ulishawahi kupanda na kufikia dola bilioni 13 kwa siku moja mwaka 2020. Inakadiriwa utajiri wake sasa una thamani ya karibu dola bilioni 200.

Mradi wake wa boti , unaofahamika kama Y721, utamalizika mwezi ujao, kwa mujibu wa Bloomberg, inasemekana kuwa Bezos aliweka oda miaka kadhaa iliyopita, kwani meli kama hizi hutengenezwa kwa miaka takribani mitano.

Vyombo hivi vya majini mara nyingi hununuliwa na mashirika kisha hukodishwa na wamiliki wa kampuni
Vyombo hivi vya majini mara nyingi hununuliwa na mashirika kisha hukodishwa na wamiliki wa kampuni

Oceanco, mtengenezaji wa boti hiyo , hajazungumza lolote kuhusu mradi huo. Awali walitengeneza boti aina ya Black Pearl ya ukubwa wa futi 350, boti ya pili kwa ukubwa duniani.

Nani hununua boti za namna hii ?

Vyombo hivi vya majini mara nyingi hununuliwa na mashirika kisha hukodishwa na wamiliki wa kampuni, hali inayofanya kuwa vigumu kusema boti ipi inamilikiwa na nani.

Katika bandari maarufu za ujenzi wa meli, kama ile ya Uholanzi ambapo Oceanco ipo, watu watajaribu kufuatilia nambari za mkia za ndege binafsi kwa jaribio la kujua ni mabilionea gani wamefika kutembelea boti yao ya baadaye.

Suala kubwa hapo ni faragha katika suala la umiliki wa boti, anasema Tucker ”soko la siri”. Mark Zuckerberg na Bill Gates, mabilionea katika nyanja ya teknolojia wanadaiwa kuwa na boti hizo.

Boti zikiwa mjini Monaco

“Hizi ni mali binafsi na moja ya sababu zinanunuliwa kwa faragha,” anasema Tucker. Faragha pia hutoa ulinzi wa usalama, si suala dogo kwa watu matajiri zaidi ulimwenguni.

Lakini licha ya umaarufu unaozidi kuongezeka, matajiri wanaweza kutaka kuweka mali zao katika hali ya usiri siku hizi.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CO4sGg9BBCX/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents