Boti yazama, watu 27 wafariki Ufaransa 

Takriban watu 27, akiwemo binti mdogo, wamefariki baada ya boti waliokuwa wakisafiri kuzama maji.

Boti hiyo ilikuwa ikielekea Uingereza ilipozama muda mfupi baada ya kuondoka kwenye bandari ya Ufaransa ya Calais.

Mashua zinazotumiwa kufanya safari kama hizo kupitia Idhaa ya Kiingereza mara nyingi ni ndogo na zinajaza watu kupita kiasi, na hivyo kkuhatarisha maisha ya watu.

Mwendesha mashtaka wa eneo hilo anasema wanawake saba na watoto watatu ni miongoni mwa waliofariki – huku watu wawili wakiokolewa.

Hakuna linalofahamika zaidi kuhusu waliokufa, uraia wao au kilichosababisha boti hiyo kuzama. Tayari Polisi wa Ufaransa wamewakamata watu watano kuhusiana na tukio hilo.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamekubaliana “kufanya kila linalowezekana kukomesha magenge yanayohusika”, lakini Johnson anasema Ufaransa inapaswa kufanya zaidi kuwazuia wahamiaji kuvuka, huku Macron akisema Uingereza inapaswa kuacha kuweka siasa katika suala hilo.

Inaelezwa waliokufa walikuwa wakimbizi wanaotaka kuelekea Uingereza.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Priti Patel amewaambia wabunge wa Uingereza kwamba ametoa ofa mpya kutoka Uingereza kuanza doria ya pamoja na Ufaransa.

Related Articles

Back to top button