Habari

Bray Sirjent kufungua mwaka na Hamisa Mobetho

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Bray Sirjent ambaye amefanya vizuri kwa mwaka 2022 anatarajia kufungua mwaka 2023 na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Hamisa Mobetho’.

Akizungumzia ujio wake huo mpya, Sirjent amesema kuwa idea ya wimbo huo itawashangaza watu wengi na pengine huenda ukawa ni moja ya nyimbo bora kwa mwaka huu kwani maudhui yake ni tofauti kidogo na jina la wimbo.

“Unajua watu wanafikiria zaidi jina la wimbo lakini hii itawashangaza sana, Wakae tuu mkao wa kula ngoma ninayo mkononi ni suala la muda tuu,” amesema @braysirgent_tz kwenye mahojiano yake na Bongo5.

Kuhusu tarehe ya kuachia kazi hiyo, Sirjent amesema anatarajia kuachia Tarehe 25/1/2023 hivyo mashabiki wake na wale wanaopenda muziki mzuri wakae karibu kwenye kurasa za mitandao yake ya kijamii.

“Nawakumbusha tuu wale wa mitandaoni napatikana YouTube, Instagram na mitandao mingine yote jina ni @braysirjent_tz wanifuate huko ili wawe wa kwanza kusikiliza Hamisa Mobetho”.

Bray Sirjent kwa mwaka Jana alifanya vizuri sana na ngoma yake ya Ntalipa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents