Michezo

Francis Cheka ahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela

Bondia mashuhuri nchini muda mfupi uliopita amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.

Bondia-Francis-Cheka

Hiyo ina maana kuwa Cheka anaenda kutumikia kifungo hicho ambapo hakimu hajatoa nafasi yoyote ya fidia.

Hukumu hiyo imetokana na kosa la bondia hiyo kumpiga meneja wake aitwaye Bahati kwenye bar ya vijana social mjini Morogoro July 2 mwaka jana alipoenda kudai fedha zake.

Meneja huyo alilazwa hospitali kufuatia tukio hilo ambapo Cheka alidaiwa kumpiga ngumi. Katika kesi hiyo Cheka alikuwa anakana mashtaka.

Bondia huyo anaenda jela huku akiwa anashikilia mkanda wa dunia wa WBF Super Middleweight.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents