Burudani

Breaking News: Sugu na Ruge wamemaliza ugomvi wao!


[Picha kwa hisani ya Angella Msangi]

Beef kali kati ya Ruge Mutahaba wa Clouds Media Group na Mbunge kijana ambaye pia ni msanii gwiji wa Hip Hop la Bongo, Joseph Mbilinyi aka Sugu, limefika kikomo baada ya wawili hao kuwekwa kikao na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Emmanuel Nchimbi na mbunge Tundu Lisu.

Wawili hao walikuwa na mzozo mkali baada ya Sugu kudai kwamba Ruge alimzunguka na kunyang’anya dili la kupiga tamasha na kampeni za kutokomeza malaria nchini kupitia wasanii mbalimbali lililojulikana kama ‘Malaria No More’, kitu ambacho kilikanushwa na Ruge siku zote.

Bifu hilo lilipeleka mpaka kugawanyika kwa baadhi ya wasanii kwenye makundi yaliyo support mmoja na kumpinga mwingine.

Bongo5 inashukuru jitihada za wote waliohusika kumaliza bifu hilo, hasa kwa sababu muziki unapaswa kutuunganisha pamoja na sio kututenganisha.

Wameonyesha upekee wa kukubali ugomvi uishe na kilichobaki sasa ni kuendeleza sanaa yetu na kuwainua wasanii wetu juu zaidi!

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents