FahamuHabari

BREAKING:Selcom yainunua Access Bank

Siku ya leo Benki ya Acces Microfinance Tanzania Limited imebadilishwa jina baada ya kuuzwa Selcom na sasa itaitwa Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited.

Akiongea na wana Habari Julius Ruwaichi Afisa Mtendaji Mkuu wa Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited.

“Tunayofuraha kutangaza hatua muhimu katika safari yetu ya kuelekea kuhudumia vyema Benki ya Access Microfinance Bank Tanzania Limited inaendelea kukua, kuimarika na kuja na mabadiliko makubwa chanya kuanzia tarehe 4, juni 2024 tutafanya kazi kwa fahari kuu chini ya jina jipya Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited.

Ubadilishaji chapa huu unaonyesha dhamira yetu ya kubadilika kulingana na mahitaji ya wateja wetu na kujielekeza kwetu kutoa huduma zilizo sahihi zaidi na fasaha za kifedha zilizojaa ubunifu mkubwa.

Kama sehemu ya kuimarisha uonekano wetu Benki ya Selcom Microfinance Tanzania Limited inaleta utambulisho mpya kwa muonekano wake na rangi kuu za muonekano wetu inabadilika ahadi zetu ni dhabiti kwako ni kutoa huduma zilizoboreshwa zinazozidi matarajio yako na kukufanya uwe nasi daima.

“Tunaelewa na kuthamini sana umuhimu wa uaminifu na utegemeo thabiti katika tasnia ya huduma za kifedha, benki yetu itaendelea kutoa ushirikiano na kuwa karibu kabisa na wateja wetu kwa kutoa huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa sekta ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania “, aliongeza Julius Ruwaichi Afisa Mtendaji Mkuu wa Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited. Tunapokumbatia utambulisho wetu mpya lengo letu linasalia katika kudumisha viwango vya juu zaidi vya uadilifu, ubunifu, uvumbuzi na huduma kwa wateja.

Tunashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono wateja wetu na tunatarajia kuwahudumia chini ya chapa ya Selcom Microfinance Bank Tanzania Limited.

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents