Brela: Mkataba wa WIPO wa ulinzi na maumbo ya michoro bunifu kutoa fursa kwa wabunifu
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imesema endapo Mkataba wa Sheria ya Kimataifa ya Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) ya Ulinzi wa Maumbo na Michoro Bunifu itapitishwa na baadaye Tanzania kuiridhia, itatoa fursa na kuongeza wigo kwa wabunifu wa Maumbo na Michoro Bunifu kusajili na kulinda bunifu zao.
Hayo yamebainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa akifungua kikao cha mashauriano ya wadau kuhusu Mkataba wa Sheria ya Kimataifa ya Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) ya Ulinzi wa Maumbo na Michoro Bunifu jijini Dar es Salaam.
“Endapo Sheria hii ya Kimataifa itapitishwa na baadaye Tanzania kuiridhia, itatoa fursa na kuongeza wigo kwa wabunifu wa Maumbo na Michoro bunifu kusajili na kulinda Maumbo na Michoro Bunifu yao katika ngazi ya Kimataifa hivyo kukuza zaidi biashara na kuwawezesha kuhimili ushindani katika masoko ya ndani na nje,” amesema Nyaisa.
Kwamba katika ngazi ya Kikanda, kupitia Itifaki ya Harare ya Ulinzi wa Hataza na Maumbo Bunifu (Harare Protocal on Patents and Dasigns) inayosimamiwa na Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO), wabunifu wamekuwa wakilinda Hataza na Maumbo ya Bunifu kupitia ARIPO yenye Makao yake Makuu Harare Zimbabwe.
Amebainisha kuwa kwa hapa nchini, upande wa Tanzania Bara, Sheria ya Ulinzi wa Maumbo Bunifu bado haiakisi mazingira ya sasa ya kusajili na kupata ulinzi wa Bunifu hizo.
Kuhusu kikao hicho cha mashauriano Nyaisa amesema kikao hicho muhimu cha wadau wa Miliki Ubunifu kinajikita katika eneo la Maumbo na Michoro Bunifu (Industrial Designs).
“Lengo la kikao hiki ni kama ambavyo mlifahamishwa awali, ni kujadili na kutoa maoni juu ya Mkataba huo wa Kimataifa ikiwa ni maandalizi ya uidhinishwaji katika mkutano wa Kidiplomasia utakaofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 12 mwaka huu huko Riyadh nchini Saudi Arabia,” amesema Nyaisa na kuongeza,
“Lengo ni kwa wadau wote kutoa maoni ikiwa ni pamoja na kupendekeza maeneo ambayo mtaona yanahitaji maboresho ili Sheria hii itakapopitishwa na Nchi wanachama iweze kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake,”.
Nyaisa ameeleza kuwa michango yao ni ya muhimu kwani itatumika kumshauri Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye ndiye mwenye dhamana ya uratibu wa Miliki Ubunifu nchini.
Pia Mustafa Haji, ambaye katika kikao hicho alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa BPRA, Khamis Juma Khamis, amelitoa rai kuwa vikao kama hivyo ni vema pia kikafanyika Zanzibar kwa lengo la kuendelea kushirikiana kwa maslahi ya taifa kwa ujumla.
Naye Mhadhiri wa UDSM, Dkt Perfect Melkiori, amesema kuwa changamoto kubwa ambayo imejitokeza kwa wanafunzi katika chuo hicho ni wengi wa wanafunzi na wafanyakazi, kutojua thamani ya bunifu zao jambo linalofanya kurubiniwa na baadhi ya kampuni na mashirika ili kuuza bunifu zao kwa bei ndogo.
Dkt Melkiori ambaye pia ni Meneja wa Miliki Bunifu wa chuo hicho, amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo kwa wanafunzi na wafanyakazi, kwa sasa wanaendelea kutoa elimu ili kuhakikisha kundi hilo halipotezi haki ya kwa kuuza bunifu kwa gaharama ndogo kutokana na kurubuniwa na kampuni na mashirika.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa BPRA Mustafa Haji, amelitoa rai kuwa vikao kama hivyo ni vema pia kikafanyika Zanzibar kwa lengo la kuendelea kushirikiana kwa maslahi ya taifa kwa ujumla.
Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Perfect Melkiori, amesema kuwa changamoto kubwa ambayo imejitokeza kwa wanafunzi katika chuo hicho ni wengi wa wanafunzi na wafanyakazi, kutojua thamani ya bunifu zao jambo linalofanya kurubiniwa na baadhi ya kampuni na mashirika ili kuuza bunifu zao kwa bei ndogo.
Dkt Melkiori ambaye pia ni Meneja wa Miliki Bunifu wa chuo hicho, amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo kwa wanafunzi na wafanyakazi, kwa sasa wanaendelea kutoa elimu ili kuhakikisha kundi hilo halipotezi haki ya kwa kuuza bunifu kwa gaharama ndogo kutokana na kurubuniwa na kampuni na mashirika.
Written by Janeth Jovin