Bruno Fernandes ndiye mchezaji hatari dhidi ya Spurs leo

- Ndiye mchezaji aliyetengeneza mabao mengi zaidi (19)
- Ushiriki wa moja kwa moja katika mabao 46
- Ametengeneza nafasi 32 katika hatua ya mtoano
Fernandes sio tu injini ya timu, bali ni mchezaji wa mechi kubwa. Akiwa na uwezo wa kusambaratisha safu yoyote ya ulinzi kwa pasi au shuti moja, uwepo wake leo unaweza kuwa tofauti kati ya huzuni na furaha kwa mashabiki wa United. Ikiwa atakuwa katika kiwango chake cha kawaida, basi Spurs wana kazi ya ziada ya kumdhibiti.
Chini ya Postecoglou, Spurs wamekuwa na matatizo mengi, lakini kutengeneza nafasi. Katika ligi luu msimu huu, licha ya kufanya vibaya ni timu nne tu zilizofunga mabao mengi zaidi, yale yasiyo ya penalti (61).
Hata hivyo, wanaingia fainali Bilbao wakikabiliwa na tatizo la kipekee: wachezaji wao watatu bora, viungo washambuliaji wote wameumia, James Maddison, Dejan Kulusevski, na Lucas Bergvall.
Pengine Yves Bissouma, Rodrigo Bentancur na Pape Sarr watakuwa na kazi kubwa kulinda safu ya ulinzi na kusaidia kupunguza madhara ya Bruno Fernandes kwenye lango lao.