HabariSiasa

Bunge lamkalia ‘kooni’ Rais Ramaphosa na mpango wa kumng’oa

Bunge la Afrika Kusini limekuwa likijadili leo hoja ya ikiwa litaanzisha mchakato wa kuamua kama Rais Cyril Ramaphosa anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi ataondolewa madarakani au la.

Ramaphosa aliyetizamwa kama mpambanaji dhidi ya rushwa baada ya mtangulizi wake ambaye utawala wake ulizongwa na kashfa za ufisadi Jacob Zuma, pia anakabiliwa na madai ya kujaribu kuficha fedha nyingi za wizi.

Ripoti ya jopo huru la uchunguzi limesema huenda Ramaphosa ana hatia ya ukiukwaji mkubwa wa sheria na utovu wa nidhamu, na hayo ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa kwenye kikao cha bunge mjini Capetown.

Chama tawala cha ANC kinamuunga mkono Ramaphosa na kimetaka jumla ya wabunge wake 230 kwenye bunge lenye wajumbe 400 kupinga kuondolewa kwake.

Upinzani umeungana kuhusu suala hilo na haijulikani ikiwa baadhi ya wabunge wa ANC, chama ambacho kimegawika, wataungana na upinzani dhidi ya Ramaphosa.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents