Burna Boy, Wizkid kuiteka Dar kwa burudani (+Video)

Wasanii wawili wakubwa nchini Nigeria, Burna Boy na Wizkid wanatarajiwa kutumbuiza Jijini Dar Es Salaam mwezi huu Novemba 2019 kwenye matukio mawili tofauti tofauti ya burudani.

Akiongea na Bongo5, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Multichoice Tanzania, Baraka Shelukindo amesema kuwa mbali na mpira,  ndani ya mwezi huu Novemba kutakuwa na matukio mawili ya burudani ya Wasafi Festival na moja litafanyika Next Door , ambapo watawaleta wasanii wawili Wizkid na Burna Boy na matamasha yote yataonekana mubashara kupitia Wasafi TV na Clouds Plus ambazo chaneli hizo zinapatikana ndani yaDStv.

Akielezea promosheni hiyo, Shelukindo amesema kuwa kampuni ya MultiChoice imekuwa na utamaduni wa kushiriki na wananchi katika kunogesha msimu wa sikukuu na kwa mwaka huu wamekuja na kampeni ijulikanayo kama ‘Shangwe za sikukuu na DStv’ ambapo ofa ya mwaka huu inahusisha kifurushi cha Compact cha mwezi mmoja pamoja na kufungiwa bila granama yoyote ya ziada.

“Kila mwisho wa mwaka tunahakikisha tunakuja na kitu kipya ili kuwahakikishia watanzania sikukuu yenye furaha zaidi. Sote tunafahamu wakati huu wa msimu wa sikukuu familia nyingi hujumuika pamoja ambapo shule huwa zimefungwa na watu wengi wakiwa katika mapumziko, huu ndio wakati muafaka wa kuwa na DStv nyumbani ambapo kuna burudani kwa kila mtu” alisema Shelukindo.

Kwa ofa hiyo mteja ana uhakika wa kifurushi cha Compact cha mwezi mzima bila malipo hivyo kuweza kushuhudia burudani kabambe zikiwemo ligikubwa ulimwenguni, katuni motomoto kwa watoto, tamthilia kabambe kama Huba, Kapuni na vipindi vingine mbalimbali bila kusahau chaneli za ndani kama vile TVE, Clouds Plus, Wasafi TV na nyinginezo.

Related Articles

Back to top button