Bwana harusi na wengine 16 wauawa na radi Bangladesh

Radi nchini Bangladesh imewapiga na kuwaua wageni 17 waliohudhuria sherehe ya harusi moja nchini humo. Watu 14 wengine ikiwemo bwanaharusi , walijeruhiwa .

Wakati huo bi harusi hakuwepo katika sherehe hiyo. Sherehe hiyo ilikuwa inafanyika katika boti moja katika mji uliopo karibu na mto wa Shigbanj, wakielekea katika nyumba ya biharusiwakati walipopigwa na radi hiyo.

Wakazi wanasema kwamba radi kadhaa zilipiga kundi hilo. Kila mwaka mamia ya watu kusini mwa bara Asia hufariki kutokana na radi.

Mwaka 2016, Bangladesh ilitangaza radi kuwa janga wakati zaidi ya watu 200 walipofariki katika mwezi wa Mei pekee, ikiwemo watu 82 katika siku moja.

Wataalamu wanasema kwamba kukatwa kwa misitu kumesababisha ongezeko la radi kutokana na kutoweka kwa miti mingi mirefu ambayo huzuia radi.

Related Articles

Back to top button