Burudani

Captain Khalid autaja ukubwa wa Diamond na Vanessa Mdee nchini Ujerumani (+video)

Mchekeshaji wa Kimataifa kutoka Bongo Captain Khalid ambaye anaishi nchini Ujerumani ameelezea ukubwa wa Diamond Platnumz na ngoma zake zinavyofanya vizuri kwenye klabu za nchini humo.

Akiongea na Bongo5, Khalid amesema Diamond ni msanii mkubwa sana hata muziki wake umefika sehemu kubwa.

Mchekeshaji huyo ameongeza kuwa hata nchini Ujerumani ukienda kwenye klabu za usiku ambazo zinacheza muziki wa Afro Beats wanacheza ngoma za Diamond, Davido, Wizkid na Vanessa Mdee.

Khalid amesisitiza kuwa wasanii hao ni wakubwa sana kwa Ulaya tofauti na watu wanavyoelewa na ndio maana Diamond amekuwa akifanya ziara za kimuziki huko.

Related Articles

Back to top button