Habari

CCM kufanya mkutano mkuu maalum Machi 12

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya mkutano mkuu maalumu Machi 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Mkutano huo unakuwa wa kwanza kwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais Dkt John Magufuli baada ya kumpokea mtangulizi wake Jakaya Kikwete. Disemba mwaka jana, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya mwenyekiti wake Rais Magufuli iliridhia mabadiliko makubwa ikiwemo kupunguza idadi ya vikao na wajumbe.

Disemba mwaka huo huo aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema baadhi ya mabadiliko hayo yanaanza mara moja na mengine yatasubiri mabadiliko ya katiba ya chama hicho.

Mbali na mabadiliko hayo, mkutano huo uliofanyika mwishoni mwaka jana ulimpitisha Rodrick Mpogolo kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (bara) akichukua nafasi ya Rajab Luhwavi ambaye aliteuliwa kuwa balozi huku Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana akiendelea na wadhifa huo kama ilivyo kwa wajumbe wengine watatu wa Sekretarieti.

Aliongea na wanahabari Alhamisi hii mjini Dodoma, Mpogolo alisema pamoja na mambo mengine mkutano huo utafanyika kutokana na mageuzi makubwa yanayofanyika ndani ya chama hicho. Naibu Katibu Mkuu huyo amesema mkutano unafanyika kufuatia mageuzi makubwa yaliyofanyika ndani ya chama hicho yanayopelekea kufanyika kwa marekebisho makubwa ya kanuni na katiba ya CCM.

“Mkutano huu pamoja na mambo mengine utafanya kazi ya kujadili na kupitisha marekebisho ya katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2012, pamoja na kanuni za chama cha mapinduzi na jumuiya zake,”alisema Mpogolo.

“Marekebisho haya ya katiba na kanuni za CCM na jumuiya zake yanafanyika kufuatia maamuzi ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyofanyika Disemba mwaka jana mjini Dar es Salaam.”

Aidha alizungumzia idadi ya wajumbe watakaoshiriki mkutano huo, Mpogolo alisema kuwa mpaka sasa bado hawana idadi kamili kutokana na uhakiki unaoendelea wa wajumbe hao.

By: Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents