CCM yaibuka kidedea uchaguzi jimbo la Konde

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeibuka na ushindi katika uchaguzi mdogo Jimbo la Konde visiwani Zanzibar, baada ya mgombea wake Sheha Faki kujipatia kura 1,796 na kuwashinda wagombea wenzake 11.

Matokeo hayo ya Uchaguzi, yametangazwa leo Julai 19, 2021, ambapo Faki amepata kura 1,796 kati ya kura halali 5,020 zilizopigwa.

Hata hivyo Chama Cha ACT-Wazalendo kimelalamikia Tume ya Uchanguzi Visiwani humo kwa kudai kuwa wamepika matokeo isivyo halali.

Uchaguzi huo mdogo umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kutokea Chama cha ACT-Wazalendo Khatib Said, kufariki dunia Mei 19 mwaka huu.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button