AfyaBurudaniHabari

Celine Dion afichua kusumbuliwa na ugonjwa usioweza kutibika

Celine Dion afichua hali ya kiafya isiyoweza kutibika ya ugonjwa nadra wa neva unaoendelea yaani Stiff Person Syndrome (SPS), yenye kujumuisha mfumo wa kinga kushambulia chembe nzuri.

Mwimbaji huyo wa Kifaransa mwenye asili ya Canada aliwaambia wafuasi wake milioni 5.2 wa Instagram hali hiyo inamfanya misuli yake kutetemeka bila kudhibitiwa.

Pia imemuacha kuwa na ugumu wa kutembea na kuimba, alisema, akimaanisha kuwa hataweza kufanya maonyesho yaliyopangwa nchini Uingereza na Ulaya mwaka ujao.

“Nimekuwa nikikabiliana na matatizo ya afya yangu kwa muda mrefu,” Dion alisema.

“Na imekuwa vigumu kwangu kukabiliana na changamoto hizi na kuzungumza juu ya kila kitu ambacho nimekuwa nikipitia,” mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 54 aliendelea kusema katika video iliyojaa hisia.

“Hivi majuzi niligunduliwa kuwa na ugonjwa wa nadra sana wa neva unaoitwa ‘stiff person syndrome’ ambao huathiri mtu mmoja kati ya milioni moja.

“Wakati bado tunajifunza juu ya hali hii adimu, sasa tunajua ugonjwa huu ndio umekuwa ukisababisha magonjwa yote ya misuli au mishipa kuanza kutetemeka ambao nimekuwa nao.”

Aliongeza: “Kwa bahati mbaya, mishtuko hii ya misuli huathiri kila nyanja ya maisha yangu ya kila siku, wakati mwingine husababisha ugumu wakati ninapotembea na kutoniruhusu kutumia sauti yangu kuimba jinsi nilivyozoea.

“Inaniuma kukuambia leo kwamba hii inamaanisha sitakuwa tayari kuanza tena ziara yangu barani Ulaya mwezi Februari.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents