Chad: Mtoto wa Idris Deby arithi kiti cha Urais baada ya kifo cha baba yake (+ Video)

Mtoto wa Idris Deby amechukua usukani wa Chad huku waasi wakiapa kuimarisha mashambulizi ya pamoja.

Kifo cha ghafla cha Rais wa Chad Idriss Deby kimemfanya mwanae , Luteni Mahamat Idris Deby Itno (al maaruafu General Kaka), kuwa kiongozi wa taifa hilo la Afrika ya kati, kwa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja kabla kufanya uchaguzi.

Waasi wanatishia kufanya upya mashambulizi dhidi ya mji mkuu N’Djamena.

Mahamat, mwenye umri wa miaka 37, jana alitangaza Baraza la Mpito la wanajeshi la wanachama 15 (TMC) linaloundwa na majenerali ambao wataiawala Chad kwa miezi 18 ijayo.

Baraza la mawaziri na Bunge lilivunjwa na amri ya kitaifa ya kutotoka nje imewekwa.Waasi kutoka chama cha Front for Change and Concord in Chad (FACT) wameripotiwa kuanza tena harakati zao kuelekea N’Djamena, baada ya kifo cha Deby.

Deby, ambaye aliongoza Chad kwa miongo mitatu, alifariki saa kadhaa baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Aprili 11 na karibu 80% ya kura.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii jana usiku, FACT ilisema: “Vikosi vya upinzaji viko katika milango ya N’Djamena.

”Tuko hapa kupiga kengele, sio za chuki au mgawanyiko, bali kupiga kengele za amani na matumaini mapya. Na zitakapolia, hakutakuwa na mikono tena nchini Chad kupiga ngoma za vita. ” ilisema taarifa hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta amewasili mjini Kinshasakatika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Felix Tshisekedi.

Uhuru amepokelewa na Rais Tshisekedi na kupewa mapokezi ya taifa na gwaride la heshima.

Katikia uwanja wa ndege Rais Kenyatta alipokelewa na Rais Tshisekedi ambaye aliambatana na maafisa wa serikali ya Congo ikiwa ni pamoja na Waziri wa mambo ya nje Christophe Lutundula na Gavana wa jiji la Kinshasa Gentiny Ngobila Mbala.

Rais Kenyatta na mwenyeji wake leo wataongoza ujumbe wao katuika mazungumzo ya ushirikiano baina ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kusaini makubaliano mbali mbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CN66sqQh-4o/

Related Articles

Back to top button