Habari

CHADEMA: Golugwa amekamatwa Airport

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kimepewa taarifa kuwa Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara Amani Golugwa amekamatwa na Jeshi la Polisi usiku wa kuamkia leo May 13, 2025 akiwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam. CHADEMA imesema Amani alikuwa anasafiri leo May 13, 2025 kuelekea Nchini Ubeljiji kukiwakilisha Chama hicho katika mkutano wa International Democracy Union (IDU) unaoanza kesho Nchini humo. “Tumezungumza na Shirika la ndege ambalo alikuwa asafiri nalo wametujuza hajafanikiwa kusafari, aliyetutuaarifu ameeleza kuwa Mhe.

Amani amepigwa sana na Jeshi hilo, pia hapatikani katika simu zake zote” “Tumetaarifiwa kuwa Mhe. Amani Golugwa yupo Kituo cha Polisi Kati Dar es salaam, Mawakili wa Chama wanaelekea kituoni hapo, tunaendelea kufuatilia tutawajuza”

 

 

cc: Millard ayo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents