Chadema waeleza kuwa Mbowe hajulikani alipo

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Freeman Mbowe ameripotiwa hajulikani alipo katika chumba chake cha hoteli jijini Mwanza.

Taarifa kupitia ukurasa wao wa Twitter inaeleza kuwa Bw Mbowe huenda amekamatwa alipokuwa akihudhuria mkutano wa chama chake cha Chadema.

Hatahivyo polisi haijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa za kukamatwa kwake

Maafisa kutoka chama chake wanasema kuwa hadi sasa hawajaweza kubaini anashikiliwa kwenye kituo kipi cha polisi.

Kulingana na taarifa ya Chadema iliyotumwa kupitia akaunti yake ya Twitter, Bw Mbowe amekamatwa pamoja na wanachama wengine 10 wa chama hicho.

Related Articles

Back to top button