Umbea

Chaney Jones awaumbua wambea wanaodai ameachana na Kanye West, apost hiki

Baada ya kusambaa taarifa za kuwa mrembo @chaneyjonesssss ameachana na @kanyewest ameamua kuvunja ukimya.

Mrembo huyo ambaye alianzisha mahusiano na Kanye West baada ya Kanye kuachana na Kim Kardashian kuanzia jana zilianza kusambaa taarifa kuwa wawili hao wameachana.

Kwani mrembo huyo alifuta picha zote Instagram na kubakisha mbili tu akiwa mwenyewe bila Kanye.

Leo asubuhi hii kupitia Insta Story yake ameamua kupost picha mbalimbali na clip akiwa na Kanye huku akimtakia siku njema ya kuzaliwa. Chaney ameandika kuwa “Happy birthday I love youuu”

Ikumbukwe kuwa @kanyewest ametimiza miaka 45 leo. post hiyo imedhihirisha kuwa wawili hao bado wapo pamoja.

Amepost hiki kupitia Insta story yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents