Habari
Chief Godlove achangia madawati 100 Mbeya

@chief_godlove amezindua mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA), Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya akiwa Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo iliyokusanya wanafunzi wa Zaidi ya Shule 120.
Akizindua Bonanza hilo Godlove ametoa Msaada wa Ng’ombe sita, Mbuzi wawili, Jezi za timu 120 na Madawati 100 ili kuweka chachu na motisha kwa wanafunzi hao.