Habari

China kutoa dozi bilioni 1 za chanjo ya Corona kwa Afrika

Rais wa China Xi Jinping ameahidi kutuma barani Afrika dozi bilioni moja za chanjo ya Covid ili kusaidia kuziba “pengo la chanjo”.

Xi Jinping alitoa ahadi hiyo wakati wa mkutano wa kilele wa China na Afrika.

Amesema kati ya bilioni moja, dozi milioni 600 zitakuwa michango kutoka China na milioni 400 zitatolewa kwa vyanzo vingine kama vile uzalishaji wa pamoja wa makampuni ya China na nchi husika za Afrika. China pia itajenga miradi 10 ya afya barani Afrika na kutuma wataalam 1,500 wa afya.

Nchi hiyo tayari imetoa takriban dozi milioni 200 kwa Afrika, huku kukiwa na wasiwasi mkubwa juu ya kuenea kwa aina mpya ya virusi Omicron, ambayo iligunduliwa kwa mara ya kwanza kusini mwa Afrika.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents