Afya

China wanaamini virusi vya Corona vilitengenezwa kambi ya kijeshi Marekani na kusambazwa makusudi

Kampeni ya propaganda nchini China kuhusu asili ya virusi vya corona inashika kasi, kabla ya kutolewa kwa ripoti ya Marekani ya ujasusi juu ya suala hilo.

Kampeni ya propaganda inasema kwamba Covid-19 ilisambaa duniani ikitokea katika kambi ya kijeshi ya Maryland nchini Marekani.

Hii inakuja baada ya Rais wa Marekani Joe Biden Mei kuagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini ikiwa virusi hivyo viliibuka kimakosa kutoka kwenye maabara, au yalikuwa ni matokeo ya mgusano baina ya binadamu na mnyama.

Tangu wakati huo, dhana kwamba virusi vya corona ”vilivuja” kutoka kwenye maabara ya Wuhan imekuwa ikipingwa na watafiti wengi , ambao waliiona kama msingi wa njama. Lakini sasa kutokana na kwamba ripoti ya ujasusi ya Marekani inakaribia kutolewa, China ilichukua msimamo mkali wa nadharia ya inayokera.

Katika kipindi cha wiki chache zilizopita, vyanzo vya habri vya China vimekuwa vikidhihaki wazo kwamba Covid -19 ilitengenezwa nchini Marekani.

Ili kueneza wazo hili, vyanzo vya China vilitumia njia na majukwaa yote- kuanzia jumbe za Facebook kwa kutumia kurasa zilizobuniwa.

Wataalamu wanaamini kuwa juhudi za kampeni hii zimefanikiwa katika kuushawishi umma wa Wachina wa ndani ya nchi kuwa na wasiwasi na taarifa yoyote ile ya kimataifa ya ukosoaji dhidi ya Uchina kuhusu mchango wake katika kusambaa kwa janga la corona.

Wamarekani wengi huenda hawajawahi kusikia jina ”Fort Detrick” ambalo linazungumziwa kote nchini China.

Waandaaji wa kampeni hii wanasambaza taarifa kwamba virusi vya Covid-19 vilitengenezwa na kuvuja kutoka kwenye ngome ya kijeshi ya Frederick, iliyopo Maryland, yapata kilomita 80 mashariki mwa Washington, DC nchini Marekani.

Ngome hii ya kijeshi awali ilikuwa ni kituo cha mpango wa silaha za kibaiolojia na sasa ni maabara ya utengenezaji wa dawa za vimelea ambako utafiti wa virusi hufanyika.

Maabara hiyo ina historia tata, ambayo ilichangia kuwepo kwa wasiwasi nchini China.

Mwanajeshi

Wimbo wa Kichina wa miondoko ya kufokafoka (rap) unasema kwamba njama ya uovu ilifanywa Marekani.

Wazo hili , linaloimbwa ndani ya wimbo huu liliidhinishwa na Wachina, alisema msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje wa China Zhao Lijian Legian ambaye anafahamika kwa mtindo wake wa matamshi yanayokera, na alituma jumbe kadhaa za Twitter kuhusu wazo hilo kusaidia kuunga mkono madai kwamba ”asili ya virusi ni Marekani”

Katika miezi ya hivi karibuni pia mabalozi kadhaa wa China katika maeneo mbali mbali duniani wamejiunga na upande wa Lijian katika kunadi mawazo haya.

”Tuko katika mchakato wa kupanua kampeni inayoendelea ya kupigia debe mawazo haya,” anasema Ira Hubert kutoka kampuni inayotathmini taarifa za mitandao ya kijamii- Graphica

Kulingana na wanaofuatilia hali ya mambo, Beijing inataka kuileta hadhira ya watu wa mataifa ya kigeni kujadili juu ya asili ya Covid-19, ikiwa ni pamoja na kile ambacho vyombo vya habari vya Uchina vimeanza kutangaza mara kwa mara, kuanzia mwezi Julai, kuhusu ujumbe wa Facebook wa mtu anayeitwa Wilson Edwards ambaye alijitambulisha kama mtafiti wa Kiswizi .

Edwards alidai katika machapisho yake kwamba, kulingana na ripoti za vyomo vya habari vya China, kuwa Washington, ambayo ilichukua jukumu la kuishambulia China kuhusu asili ya virusi vya covid, haitaki kufungua macho yake kuona taarifa na data.

Lakini ubalozi wa Uswizi nchini China baadaye ulisema kwamba rekodi rasmi za nchi hiyo hazikuwa na jina la raia wake mwenye jina Wilson Edwards, na badala yake ubalozi ulivitaka vyombo vya habari vya Uchina kuachana na taarifa ”zisizo sahihi”.

Credit by BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents