Habari

China yadai imeionya meli ya kivita ya Marekani katika bahari ya kusini

Jeshi la China limesema leo kuwa vikosi vyake viliionya meli ya kivita ya Marekani iliyoingia karibu na visiwa vya Paracel katika bahari ya China Kusini, katika ongezeko la karibuni zaidi la mzozo juu ya njia ya bahari inayozozaniwa.

Kamandi ya kusini ya jeshi la China imesema meli ya Marekani ya USS Benfold, ilisafiria kinyume cha sheria katika sehemu ya China bila ruksa, na kukiuka mamlaka ya taifa hilo, na kwamba vikosi vya majini na angani vya China viliifuatilia meli hiyo.

Jeshi la majini la Marekani limesema hata hivyo kwamba meli yake ilishikilia haki za ubaharia na uhuru karibu na kisiwa cha Paracel, kwa kufuata sheria ya kimataifa.

Marekani hufanya mara kwa mara kile inachokiita safari za uhuru wa ubaharia katika bahari ya China Kusini ili kupinga madai ya China juu ya maeneo ya bahari hiyo, ambako imejenga visiw kadhaa na kuweka vituo vya kijeshi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents