Uncategorized

China yatoa onyo kwa raia wake kuondoka mashariki mwa Congo

Ubalozi wa China nchini DR Congo umewataka raia wake kuhama majimbo matatu yaliyoko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo haraka iwezekanavyo.

Ujumbe kutoka ubalozi wake wa Kinshasa unasema kuwa idadi kubwa ya raia wa China wamekuwa wakishambuliwa na kutekwa kwa mwezi mmoja sasa kutoka majimbo ya matatu ya Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Ituri mahala ambapo kumewa na visa kadhaa vya wizi wa kutumia silaha.

Raia wa Uchina kutoka maeneo hayo wametakiwa kuripoti katika ubalozi ifikapo tarehe 10 Disemba “Tunaomba raia wote wa China na wafanyabiashara waliowekeza Congo tafadhali wazingatie hali ya ndani, waongeze ufahamu wao wa usalama na kujitayarisha kwa dharura na kuepuka safari za nje zisizo za lazima.” imesema Ubalozi huo.

Hakuna taarifa za matukio zilizotolewa ingawaje Ubalozi huo mwezi uliyopita waliripoti kuwa raia watano wa China walitekwa nyara huko Kusini mwa Kivu katika shughuli za uchimbaji madini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents