Clouds media watolea ufafanuzi mil 629.7 zilizotajwa na CAG (+ Video)

Meneja wa Fedha wa Clouds Media Group, Bw. Issa Masoud, amesema Clouds ilitoa vielelezo vyote ikiwa ni pamoja na stakabadhi kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, kufuatia malipo ya shilingi milioni 629.7 kwa ajili ya matangazo ya Tamasha la Urithi mwaka 2018.

Bw. Masoud ametoa taarifa hiyo kupitia Kipindi cha Traffik Jamz kinachorushwa na Clouds Fm, ikiwa ni saa chache baada ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuwasilisha ripoti ya ukaguzi, inayoonyesha Clouds Media Group kulipwa kiasi hicho cha fedha, lakini hakuna risiti zinazothibitisha malipo hayo!

 

Related Articles

Back to top button