HabariSiasa

Congo yazitaka Arsenal na PSG kufuta neno Visit Rwanda kwenye jezio zao

Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeziandikia timu za soka barani Ulaya zinazopata ufadhili kutoka serikali ya Rwanda kutopokea, ‘Fedha zinazotokana na umwagikaji wa damu,’ unaoendelea mashariki mwa DRC.

Kulingana na DRC, Waziri wake wa mambo ya kigeni Therese Kayikwamba Wagner ameziandikia klabu za Arsenal FC ya Uingereza, Paris Sint-Germaine ya Ufaransa na FC Bayern Munich ya Ujerumani kusitisha ushirikiano wao wa ufadhili wa mauzo chini ya mpango wa, ‘Visit Rwanda,’ wakidai kwamba idadi kubwa ya wanajeshi wa Rwanda wanapigana na jeshi la FARDC huko Goma wakisaidiana na kundi la waasi la M23.

Katika barua yake kwa klabu ya Arsenal ya Uingereza Waziri Wagner amesema kwamba, ‘Rwanda inastahili kulaumiwa kwa hatua zake ndani ya DRC kwani Umoja wa mataifa umeripoti kwamba kikosi cha wanajeshi 4,000 kutoka Rwanda kiko ndani ya DRC na kinashikriki kwenye vita vinavyoendelea nchini humo.’

Na huku klabu hizo zikisubiriwa kufanya uamuzi kuhusu ombi hilo la DRC na shutuma dhidi ya Rwanda, DRC imeendelea kuwasilisha hoja yao ya hali mbaya inayoshuhudiwa mashariki mwa nchi hiyo.

.Chanzo cha picha,Bayern Munich
Maelezo ya picha,Kutoka kushoto kwenda kulia: Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB) Clare Akamanzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Bayern Jan-Christian Dreesen na Waziri wa Michezo wa Rwanda Aurore Mimosa Munyangaju
Waziri Wagner ameiambia klabu ya Arsenal kwamba, ‘ Maelfu ya watu wamekwama jijini Goma, ambapo hakuna njia ya kuingiza chakula, huku huduma za kusambaza maji na umeme zikiwa zimekatizwa. Hakuna usalama, watu wameuawa na wizi unakithiri mjini. Mfadhili wenu anahusika moja kwa moja kwa mahangaiko haya ya wengi.’

Barua hiyo inaangazia mpango wa, ‘VISIT RWANDA’ unafadhiliwa moja kwa moja na uchimbaji madini haramu unaoendelea katika maeneo kadhaa yaliyokaliwa mashariki mwa DRC na kuvukishwa mpaka hadi Rwanda ambayo inasafirisha ughaibuni kama madini yake asilii.

Rwanda imekanusha mara kwa mara kuhusika na kundi la M23 au kuchimba madini katika jimbo la Kivu Kaskazini kinyume na sheria za DRC au zile za kimataifa.

Lakini, Ripoti iliyochapishwa mwishoni mwa 2024, na Umoja wa Mataifa imeripoti kwamba tani 150 za madini ya Coltan kutoka DRC yalikuwa yakichanganywa na yale kutoka Rwanda na kusafirishwa hadi ughaibuni katika kashfa kubwa ya kuchanganya madini kutoka eneo la maziwa makuu.

DRC inakadiria kwamba thamani ya madini ambayo Rwanda inadaiwa kuchukuwa kinyume na sheria kutoka DRC ni takriban dola bilioni moja ya Uchumi wa nchi hiyo. Kwa sababu hiyo, DRC sasa inataka klabu za Ulaya ambazo zinapokea ufadhili wa mauzo kukata uhusiano na Rwanda.

Kutokana na tishio la Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Larmmy, kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda, kwamba Uingereza huenda ikasitisha ufadhili wa takriban dola bilioni moja za kimarekani , DRC katika barua yake pia imezitaka klabu hizo za Soka kufanya uchunguzi kuhusu chanzo cha ufadhili na ushirikiano wanaokuwa nao na Rwanda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents