FahamuHabariLifestyleMichezo

Ronaldo anapangisha jumba lake $10,980, sawa na Tsh milioni 25 kwa mwezi

Nyota wa klabu ya Alnassr na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuwa anakodisha/pangisha jumba lake la Kifahari lililopo katika jiji la Madrid nchini Unispania kwa euro 10,000 tu (takriban $10,980) sawa na Tsha 25,726,140/= ( Milioni 25 za Kitanzania ) kwa mwezi!

Jumba hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 43,000 linaelezwa kuwa lina vyumba saba vya kulala, bafu tisa, mabwawa mawili ya kuogelea, (Swimming Pool) uwanja wa mpira wa miguu, na kituo cha mazoezi ya viungo vya hali ya juu (Gym) na baadhi ya miongoni mwa maeneo mengine ya kifahari kama chumba cha Cinema na mengine.

Jumba hilo la Kifahari la Ronaldo linaelezwa kuwa ni miongoni mwa majumba ya Kifahari zaidi huku likiwa na paking ya magari ya ndani.

Kupitia mtandao wa @archdaily watu wengi wameweka comment zao wakidai kiasi hicho ni kidogo sawa kutokana na namna jumba hilo la Ronaldo lilivyofafanuliwa ukubwa wake.

Kwa upande wake chumba/nyumba ya kiasi gani ndio mwisho wako kupanga na Je unahisi kiasi kilichowekwa ni sahihi??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents