Habari

CWT Iringa yawaonya Walimu wenye mahusiano ya kingono na Wanafunzi

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akipokea hotuba ya walimu wa Iringa Vijijini wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho.
Fredy Mgunda,Iringa.

CHAMA Cha Walimu Wilaya ya Iringa vijijini (CWT) kimeonya kuwa hakitohusika na utetezi Wa Waalimu watakaojihusisha na vitendo vya utovu Wa nidham ikiwemo mahusiano ya kingono na wanafunzi.

Mwenyekiti Wa CWT Wilaya ya Iringa Vijijini Mwalimu Simoni Mnyawami amesema ni aibu kusikia waalimu wakitajwa kuhusika uhalifu huo huku akisisitiza hatua zaidi za kisheria zichukuliwe ili iwe fundisho Kwa watakaobainika.

Mwenyekiti huyo ameyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa CWT baada ya Mgeni wa Heshima mkuu wa wilaya ya Iringa kuwataka waalimu kuzingatia weledi wa taaluma kwa kuwafifichua wanaojihusisha kingono na wanafunzi.

Mnyawami alisema kuwa suala la utovu wa nidhamu linapaswa kuheshimuwa kwa kila mwalimu ili kulinda hadhi ya taaluma hiyo Ikiwemo Utoro, ulevi wa kupindukia pampja na baadhi ya waalimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.

Mwenyeji wa Mkutano Huu mkuu wa kikatiba Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Iringa vijijini Mwl Simoni Mnyawami alisema ni muhimu waalimu akatambua na kuheshimu taaluma waliyo nayo Kwa kuwa wamepewa dhamana na serikali pamoja na jamii kuwa walezi wa watoto katika kuwajenga kinidham na kitaaluma.

 

Kulingana na Changamoto ya utovu wa nidham unaotajwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo aliyekuwa Mgeni wa heshima anasema jambo la walimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi halipaswi kufumbiwa macho

Moyo amewataka walimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanafunzi wanaowafundisha ili taifa liweze
kupata wasomi wengi ambao wanauwezo wa kuja kukisaidia Taifa hapo baadae.

Alisema kuwa Kuna baadhi ya walimu wamekuwa wakiaribu taswira halisi ya kada ya ualimu kwa baadhi ya walimu kufanya mapenzi na wanafunzi na uwafanyia ukatili wanafunzi kwa makusudi hivyo walimu wanapaswa kutoa taarifa kwa mwalimu yeyeto atakayekutwa anafanya vitendo vya ukatili.

Alisema kuwa kazi kubwa ya mwalimu ni kuwafundisha wanafunzi waweze kufaulu na sio kuwafanyia ukatili wanafunzi..

Aidha Moyo alimazia kwa kusema kuwa walimu wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa wamekuwa wanafanya vizuri kwenye kufundisha wanafunzi ndio maana matokeo yake yamaekuwa mazuri mwaka hadi mwaka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents