Afya

Daktari afumua kidonda cha mgonjwa baada ya kukishona kisa hana pesa ya kulipa, Serikali yatoa tamko (+ Video)

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema video inayosambaa mitandaoni ikimuonyesha daktari aliyemshona jeraha mgonjwa na kufumua mshono kwa madai ya kushindwa kulipa gharama ni tukio lililotokea Julai, 2021.

Imesema lilitokea katika kituo cha afya Kerenge kilichopo tarafa ya Magoma halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Ufafanuzi huo umetolewa leo Jumamosi Septemba 4, 2021 baada ya kusambaa kwa video hiyo na kuzua mjadala mtandaoni huku Wizara ya Afya ikitoa tamko na kuomba mwenye kufahamu eneo husika kutoa taarifa na kisha kuweka namba ya simu.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo naibu katibu mkuu Tamisemi anayeshughulikia afya, Dk Grace Magembe amemtaja mtumishi aliyekiuka miiko ya udaktari kuwa ni Dk Jackson Meli ambaye ni ofisa wa kituo hicho cha umma.

“Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ameshachukua hatua kwa kumsimamisha kazi na amempa hati ya mashtaka na pia ameshafikishwa kwenye baraza la madaktari ili achukuliwe hatua stahiki kwa kwenda kinyume na miiko ya taaluma ya udaktari,” amesema Dk Magembe.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents