Habari

Daktari amkata mgonjwa mguu usiostahili kukatwa, Austria

Australia – Daktari mmoja wa upasuaji nchini humo amepigwa faini baada ya kumkata mguu ambao haukufaa kukatwa mgonjwa mmoja mapema mwaka huu.

Mguu wa kulia wa mgonjwa huyo ulitolewa badala ya wa kushoto, na kosa hilo liligunduliwa siku mbili baadaye.

Siku ya Jumatano, mahakama ya Linz ilimpata daktari mwenye umri wa miaka 43 na hatia ya uzembe mkubwa na kumtoza faini ya Euro 2,700 (£2,296).

Mjane wa mgonjwa huyo, ambaye alifariki dunia kabla ya kesi kufika mahakamani, pia alitunukiwa euro 5,000 kama fidia.

Mgonjwa huyo alihudhuria kliniki ya Freistadt Mei mwaka jana ili kukatwa mguu lakini daktari wa upasuaji aliweka alama katika mguu usio sahihi ili ukatwe shirika la habari la AFP linaripoti.

Kosa liligunduliwa wakati wa kubadilisha bendeji ya kawaida na mgonjwa aliambiwa atalazimika kukatwa mguu wake mwingine pia.

Wakati huo, hospitali ilisema tukio hilo limetokea kama “matokeo ya msururu wa hali mbaya”. Mkurugenzi wake aliomba msamaha hadharani katika mkutano wa wanahabari.

Mahakamani, daktari wa upasuaji alisema kumekuwa na dosari katika msururu wa utoaji wa amri katika chumba cha upasuaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents