AfyaFahamu

Daktari: Shisha moja ni Sigara 100

Baada ya kuwepo kwa mwamko mkubwa wa matumizi ya vilevi na vitu vingine vinavyochochea Ubongo ni miongoni mwa changamoto kubwa ya kushamiri magonjwa ya afya ya akili nchini na sehemu nyingine Duniani.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya figo, Garvin Kweka wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ameeleza haya kwenye mada yake ya mahusiano ya magonjwa na afya ya akili, takati wa mafunzo ya uongozi kwa Viongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).

Dkt Kaweka ambaye pia ni mtaalamu wa magonjwa ya Afya ya akili amesema kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kati ya watu wanne, mmoja wao ana changamoto ya Afya ya Akili.

Amesema hivi sasa wanawake wengi wanatumia vilevi kupindukia ikiwemo uvutaji wa shisha kwa muda mwingi na kwamba uvutaji shisha saa moja pekee ni sawa na uvutaji wa Sigara 100, kitendo hicho ni kuhatarisha Ubongo, Figo na Ini.

 

Chanzo: TanzaniaWeb.Live

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents