HabariVideos

Dar: Fundi simu mbaroni kwa mauaji ya Mwanamke (Video)

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linamshikilia Heri Julius Chisanga, umri 33, Myao fundi simu na mkazi wa Mburahati kwa tuhuma za kumuua Leonia Julius Ziota miaka 35, Mnyamwezi, mkazi wa Sinza, Msusi katika saluni iliyopo maeneo ya Sinza Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Tukio hilo lilitokea tarehe 17/06/2022 ndani ya moja wapo ya chumba katika Nyumba ya kulala wageni iitwayo Lavi Park iliyopo maeneo ya Tegeta kwa Ndevu Kinondoni Jijini Dar es Salaam, ambapo mwili wa Marehemu ulikutwa ndani ya chumba hicho.

Chanzo halisi cha tukio hilo kinachunguzwa, na kwa kutumia mbinu za Upelelezi wa kisayansi Mtuhumiwa huyo aliyetoroka mara baada ya tukio hilo amekamatwa tarehe 21/06/2022 maeneo ya Manzese Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam linatoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayetenda kosa la jinai atafuatiliwa mpaka akamatwe na kufikishwa kwenye mifumo ya haki ya kisheria.

Related Articles

Back to top button