Burudani
Davido amshushia tuhuma nzito R. Kelly
Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido ameonesha msimamo wake juu ya sakata la udhalilishaji kingono linalomkabili R. Kelly.
Davido akimjibu moja ya mashabiki wake kwenye mtandao wa Twitter, amesema kuwa hakuwepo kipindi hicho lakini inavyoonekana tu kwenye video R. Kelly anaonekana alifanya vitendo hivyo.
Aliulizwa hivi na shabiki huyo “unadhani ni kweli R. Kelly amefanya uchafu huu (unyannyasaji kingono) unaozungumzwa?” na Davido naye akajibu “Sikuwepo, lakini inavyoonekana tu jamaa anaonekana alifanya” .
Kwa sasa R. Kelly yupo kwenye uchunguzi nchini Marekani, juu ya tuhuma za unyanyasaji wanawake kingono zinazomkabili.