Habari

DAWASA yatangaza upungufu huduma ya maji kwa wakazi wa Dar- es- Salaam, Pwani

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia Wateja na wananchi wa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani kuwa kumekuwa na upungufu wa huduma ya maji kutokana na hitilafu ya umeme katika mfumo wa kupokea umeme kwenye mtambo wa uzalishaji Maji wa Ruvu Juu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro amesema kuwa maeneo yanayoathirika ni maeneo yote Mlandizi, Msufini, Vigwaza, Chamakweza, Ruvu, Kwa Mathias, Pangani Bokomnemela, Kibaha, Visiga, Picha ya Ndege, Kiluvya, Kibamba.

Amesema maeneo mengine ambayo yatakosa maji ni Mbezi, Makabe, Kimara, Msewe, Changanyikeni, Mabibo, Kisarawe, Ukonga, Kinyerezi, Tabata, Temeke, Segerea, Makuburi, Ubungo Maziwa, Mwananchi, Kiwalani, Lumo, Yombo Vituka, Uwanja wa Ndege, Banana, Viwanda vya Barabara ya Nyerere, Jet, Buguruni pamoja na TAZARA.

Lyaro amesema kuwa wataalam wa DAWASA na TANESCO wanashirikiana ili kurudisha huduma ya maji katika hali ya kawaida hivyo wanawaomba wananchi wawe wavumilivu wakati wataalam wanaendelea na jitihadi za kurudisha huduma hiyo.

“Wateja wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 00800110064 (bure) au 0735 202-121 (WhatsApp tu),” ameeleza Lyaro katika taarifa hiyo

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents