Habari

DC Namtumbo awaasa wananchi kushiriki mapokezi ya Mwenge Mei 15, mwaka huu

Wananchi wa Namtumbo wameaswa kujitokeza kwa wingi ili kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa tarehe 15 mei 2025.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji Cha Mkongo na Msindo Vilivyopo kata ya Lusewa Wilaya ya Namtumbo, Mkoani Ruvuma.

DC Malenya, Aliwasisitiza wananchi hao kuwa, Mwenge wa Uhuru ni tukio muhimu la kitaifa linalolenga kuhamasisha maendeleo, kuimarisha mshikamano wa kitaifa na kukuza uzalendo miongoni mwa Watanzania

“Ni muhimu wananchi wote wakajitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru. Huu ni mwenge unaomulika maendeleo ya taifa letu, na ni fursa ya kuonesha mshikamano, uzalendo na dhamira ya kushiriki katika ujenzi wa taifa.”

Aidha Malenya aliwataka pia viongozi wa mitaa na vijiji kushirikiana kikamilifu katika maandalizi ya mapokezi hayo, kuhakikisha usalama na mshikamano unazingatiwa ili kufanikisha tukio hilo muhimu kwa mafanikio makubwa.

Maandalizi mbalimbali yameanza kufanyika ili kuukaribisha Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Namtumbo

Written by Angel Kayombo, Ruvuma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents