Habari

Diamond alivyokutana na Mwenezi CCM Taifa Shaka, aeleza alichozungumza (Picha)

Msanii ghali wa muziki na CEO wa WCB, Diamond Platnumz wiki alitembelea Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Mpya wa CCM Ndugu yangu Shaka na kufanya naye mazungumzo.

”Wakati mzuri leo katika Ofisi Ndogo a Hamdu Shaka. @shakazulu36
Nimetumia wakati huo kumng’ata sikio juu ya matarajio yetu kwa Chama na Serikali katika Sekta ya Habari, Sanaa na Burudani, na amenihakikishia changamoto zote zitafanyiwa kazi na tabasamu litazidi kuonekana
Mwisho, Kama Kijana nimefarijika kuona Mwenyekiti wangu wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani anaendelea kuamini Vijana katika nafasi mbalimbali za Uongozi ndani ya Chama na Serikali, Katibu Mkuu wa CCM Kijana, Mwenezi Taifa wa CCM Kijana hili lina maana kubwa katika hili na mpongeza sana na ninawaomba Vijana na Watanzania wote wenzangu tumuunge Mkono, Mhe. Samia Suluhu Hassani ili mazuri aliyoyapanga katika Uongozi wake yaweze kutimia.” @diamondplatnumz

 

Related Articles

Back to top button